TARI YAANZA KAZI YA UOTESHAJI WA MICHE YA ZAO LA MKONGE KWA NJIA YA MAABARA

Baadhi ya miche ya mkonge iliyooteshwa maabara
Happiness Tesha, Kigoma
Kituo cha utafiti wa Kilimo TARI kimeanza kazi ya uoteshaji wa miche ya zao la mkonge kwa njia ya Maabara ili kusaidia upatikanaji wa mbegu bora zinazo himili magonjwa na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa sehemu ya mkakati wa kufufua kilimo cha zao hilo.
uwekezaji katika Kilimo ikiwemo teknolojia zinazosaidia kuongeza uzalishaji ni miongoni mwa suala linalosisitizwa na wadau wengi katika kukuza sekta hiyo, anasema Pascal Sulley Mchambuzi wa Uchumi.
Mbegu bora katika Kilimo ni miongoni mwa changamoto kwa wakulima wengi,vivyo hivyo katika zao la mkonge, bado njia za kawaida za kupata mbegu bora za zina changamoto nyingi ikiwemo ubora na uhimili wa magonjwa, hivyo njia ya kuotesha kupitia Maabara inaondoa hayo kama anavyoeleza Dr Fred Tairo, Meneja wa kituo cha utafiti cha TARI Dar Mikocheni

Dkt Fred Tairo ambaye ni meneja wa kituo cha TARI Mwenge Jijini Dar Es Salaam akionyesha miche ya mkonge ambayo imeoteshwa kutoka katika maabara hiyo.
Anasema njia hiyo pia inasaidia kuzalisha miche mingi kwa mara moja na katika kipindi kifupi tofauti na njia za asili ambazo itakulazimu kusubiri hadi miaka 10 kupata mbegu na kwamba mche uliofikisha miezi 12 ndio unaotumika kuotesha miche mingine maabara.
“Baada ya kuwekwa katika chumba hiki maalum kwa ajili ya kukuza mimea, Itakaa kwa mwezi mmoja na kukatwa ili kuongeza idadi ya miche zaidi kabla ya kupelekwa kwenye kitalu nje ya maabara tayari kwa kupandwa kama anavyoeleza,”MagrethLupembe mtafiti katika kituo hocho anaelezea.

Miche ya mikonge ikiwa maabara inaotesha
Mtafiti Magreth anasema huu ni mkakati maalum wa kusadia kufufua Kilimo cha zao la Mkonge kama sehemu ya juhudi za Tanzania kutaka kufanya mageuzi kwenye kilimo sekta ambayo bado ina changamoto nyingi.
Hivi karibuni akizungumza katika uzinduzi wa mchakato wa kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo, Makamu wa Rais wa Tanzania Dr Philip Mpango ametaka Tanzania kuikumbatia teknolojia katika Nyanja zote za uzalishaji.

Mtafiti na Mtaalamu wa maabara Magreth Lupembe akikagua shina la mkonge.
Zao la mkonge ni miongoni mwa mazao ya kimkakati ya Kibiashara hapa Tanzania ambayo jitihada za kuongeza uzalishaji wake zimekua zikiendelea japo wadau wa zao la Mkonge wakitaka hatua zaidi kukuza kilimo hicho chenye soko la uhakika huko nchini China na Saudi Arabia.