TUMIENI VITAMBULISHO HIVYO KAMA FURSA YA KUKUA KIUCHUMI.

Na Mwandishi Wetu, Kigoma.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma, Vumilia Julius Simbeye amewataka wajasiriamali wadogo kutumia vitambulisho walivyopewa kutafutia fursa za kuwawezesha kukua kiuchumi

Ameyasema hayo wakati akigawa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo leo katika ukumbi wa Halmashauri huku takribani vitambulishio 80 vimetolewa ikiwa ni awamu ya pili ya zoezi la ugawaji vitambulisho hivyo.

Ameeleza kuwa vitambulisho hivyo vitawapa fursa ya kutambulika lakini pia kutumika kama kigezo kikubwa cha kukopesheka kwa wajasiriamali hao hivyo kutumia mikopo hio kukua katika biashara zao.

“leo tukabidhiane vitambulisho hivi kesho tukutambue kama mzabuni ambae anaweza kutuhudumia katika miradi mbali mbali inayotekelezwa na serikali yetu.”

Aidha zoezi hilo limeambata na utoaji wa elimu ya ujasiria mali lakini pia elimu ya fedha iliyotolewa na benki ya NMB tawi la Kasulu ikiwemo fursa za mikopo zinazotolewa na benki hiyo.

Ikumbukwe kuwa ugawaji wa vitambulisho vya ujasiriamali zoezi linaloendelea baada ya uboreshwaji wa vitambulisho vilivyokuwa vinatolewa awali ikiwemo kudumu kwa miaka mitatu lakini pia kutoa vipaombele katika ugawaji wa mikopo na kuwatambua wajasiriamali wadogo hapa nchini.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )