MAHAKAMA YATAKIWA KUSHUGHULIKIA HARAKA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA


Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dk Rashid Chuachua amewataka watendaji wa mahakama kuharakisha kufanyia kazi kesi za ukatili wa kijinsia zinazofika mahakamani

Dk Chuachua ameyasema hayo wakati akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye katika maadhimisho ya siku ya familia kwa jeshi la Polisi na kusisitiza kwamba Kwa kufanya hvyo matukio hayo yatapungua.

Amesema juhudi zinahitajika ili kutokomeza matukio hayo kwa ushirikiano kati ya jeshi la polisi, jamii na mahakama.

Akisoma risala kwaniaba ya Jeshi la polisi kwa mgeni rasmi, Koplo Julias Ntandu amesema takribani kesi 1760 za ukatili wa kijinsia zimelipotiwa katika dawati la jinsia ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 ukilinganisha na mwakanuliopita.

Ameongeza kuwa, jeshi hilo linaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu kuripoti matukio ya ukatili wakijinsia kwani imani ya jeshi hilo ni kuwa bado kuna matukio mengi ambayo hayaripotiwi.

Ameongeza kuwa, changamoto kubwa inayowakabili katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijisia ni matukio mengi kutendeka ndani ya familia ambayo ni takribani asilimia 60.

Kuhusu matukio ya uvunjifu wa sheria Koplo Ntandu amesema, jeshi hilo limefanikiwa kupunguza matukio hayo kwa takribani asilimia 23 ikiwemo Uhalifu na ujambazi wa kutumia silaha ambapo waharifu takribani 1200 wamekamatwa kwa mwaka 2024.

Aidha Koplo Ntandu amesema, ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 15 na madereva takribani 450 wamekamatwa na kufikishwa mahakami ambapo wamepewa adhabu mbalimbali ikiwemo kulipa faini au vifungo gerezani.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )