WANANCHI KIGOMA UJIJI KUNUFAIKA NA MIKOPO ISIYO NA RIBA KUTOKA CRDB BANK
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Hashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Benki ya CRDB zimesaini mkataba kwa ajili ya utoaji mikopo isiyokuwa na riba kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Hafla hiyo imefanyika baina ya Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na uongozi wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma yakishuhudiwa na Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa.
Mikataba hiyo imesainiwa kwa Halmashauri kumi (10) ili kuwahudumia Wananchi kikamilifu kupunguza umasikini na kujiongezea kipato.
Halmashauri zingine zilizosaini Mikataba ni pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, Jiji la Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Halmashauri ya Bumbuli, Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na Halmashauri ya Itilima.