HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MIFUPA, UBONGO SASA KUPATIKANA NYANDA ZA JUU KUSINI

Na Mwandishi Wetu, Iringa

Serikali kupitia Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imedharia kuzisogeza huduma za kibingwa za mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kupitia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tosamaganga, mkoani Iringa.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tosamaganga Padri Benjamini Mfaume, Februari 13, 2024 wakati wa zoezi la usimamizi shirikishi linaloendeshwa hospitalini hapo na na wataalam kutoka Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Timu za Afya za ngazi ya mkoa na wilaya.

Padri. Mfaume ambaye pia ni Daktari bingwa wa Masuala ya Mifupa, amesema hospitali hiyo kwa siku za hivi karibuni mahusiano baina yake na hospitali ya MOI yameimarika zaidi lengo likiwa kujengeana uwezo na kusogeza huduma hiyo eneo laNyanda za Juu Kusini.

“Hospitali yetu kwa kushirikiana na Serikali iko mbioni kunzisha, kuboresha na kudumisha huduma za wagonjwa mahututi (ICU) ili kuokoa maisha ya watu wanaotoka eneo hilo na maeneo ya jirani,” amesema Dkt. Mfaume kuongeza.

Ameongeza kuwa huduma hiyo itakuwa na vitanda 18 kwa kuanzia na inahitajika pia kuweka mfumo wa huduma za oksijeni ili pia wateja wapate huduma hiyo,

Amesema, kwa kushirikiana na Serikali wanatarajia kulikamilisha suala hilo hivi karibuni, na ni imani yao kuwa kwa kushirikiana na Serikaali yote haya yataboreshwa likiwemo eneo la maama na mtoto.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )