TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu Andengenye amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za umma na binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo, akibainisha kuwa huduma bora za maji na usafi wa mazingira ni msingi wa ustawi wa jamii na uchumi wa mkoa.

Amezungumza hayo kikao muhimu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kigoma (RCC) kilicholenga kujadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 huku Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA) ikiwa sehemu ya washiriki.

Kikao hicho kilichofanyika chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Jenerali Mstaafu Thobias Andengenye, kimewakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa maendeleo na taasisi muhimu zenye mchango mkubwa katika maendeleo ya mkoa huo.

Kikao hicho pia kilijadili vipaumbele vingine vya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kikilenga kuboresha maisha ya wakazi wa Kigoma kupitia utekelezaji wa miradi yenye tija na endelevu.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )