TUENDELEZE USHIRIKIANO WA KIIMANI ULIOPO: DC KIGOMA

Na Mwandishi Wetu, Kigoma 

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma amewataka Wananchi na Wakazi wa Wilaya hiyo kuendeleza umoja na mshikamano wa Kiimani uliopo Nchini Tanzania.

Ameyasema hayo Leo March 24, 2025 katika Iftari iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ukumbi wa Kigoma Social Hall huku akiwataka Wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kukuza maendeleo ya Mji.

Aidha amewataka kuendelea kuombea amani na Viongozi wa Nchi akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan.

Iftari hiyo imehudhuriwa na Shekhe wa Mkoa, Katibu Baraza la Bakwata Mkoa, Wajumbe wa Baraza la Mashekhe Bakwata Mkoa, Mwakilishi wa Shekhe wa Wilaya, Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi na Waalikwa mbalimbali.

 

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )