MKUU WA MKOA KIGOMA BALOZI SIRRO AKABIDHIWA OFISI
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amekabidhi Ofisi kwa Mkuu wa Mkoa Mpya wa Kigoma Balozi Simoni Sirro mara baada ya mabadiliko ya Uongozi yaliyofanywa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan hivi Karibuni.
Hafla ya Makabidhiano imefanyika Leo Julai 2, 2025 katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa zikihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Kisiasa, Viongozi dini, Waandishi wa habari pamoja na Wananchi.