MKUU WA MKOA KIGOMA ASISITIZA KUTENGWA MAENEO YA UWEKEZAJI

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Nyakolo Sirro amesisitiza kutengwa kwa maeneo ya uwekezaji pamoja na kuwezesha wananchi kufanya biashara.

Amesema hayo wilayani Kakonko ikiwa ni katika mwendelezo wa ziara yake katika halmashauri zote mkoani Kigoma inayolenga kuzungumza na watumishi wa umma pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.

Amesisitiza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ikiwemo zao la parachichi kwa ajili ya kuvutia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Evance Malasa amesema licha ya mafanikio ya kiuchumi  yanayopatikana bado kuna changamoto miunombinu ya barabara inayounganisha Kakonko na nchi jirani ya Burundi.

Akiwa Wilayani Kakonko Balozi Sirro, ametembelea ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo, pamoja na ujenzi wa jengo la kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya na kuelekeza kuwa jengo hilo lianze kufanya kazi kuanzia Agosti Mosi mwaka huu.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )