SHIRIKA LA AIRD NA KGPC KUINGIA MAKUBALIANO YA KIUTENDAJI


Shirika la African Initiatives for Relief and Development- (AIRD) na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kigoma-KGPC wanataraji kuingia hati ya makubaliano (MOU) kwa ajili ya kuboresha mahusiano ya kikazi nakuwezesha kuripoti hababri zinazohusu wakimbizi nchini.

Hatua hiyo inafuatia pande hizo mbili kukutana ofisi za KGPC leo kwa ajili ya kuweka msingi wa kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha shughuli zinazofanywa na shirika hilo zinakuwa wazi kwa kushirikiana na KGPC.

Akizungumza wakati wa kikao hicho afisa mawasiliano na masoko wa shirika hilo Muhwezi Charlotte amesema huenda wakaingia makubaliano hayo mapema wiki ijayo.

Charlote amesema Shirika linajihusisha na masuala ya wakimbizi katika kambi zilizopo nchini kwa ufadhili wa shirika la United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR) ambapo Makamu Mwenyekiti wa KGPC Jacob Ruvilo amesisitiza adhima ya waandishi wa habari kutumia nafasi hiyo kuandika habari hizo kwa kina kwaa maslahi ya nchi

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )