DRC YATARAJIA DOZI ZA CHANJO YA MPOX TAREHE 5 SEPTEMBA
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inatarajia dozi zake za kwanza za chanjo ya mpox siku ya Alhamisi, 5 Septemba.
Kundi la kwanza litakuwa na dozi 99,100. La pili litakuwa na dozi 100,900 siku ya Jumamosi, Septemba7.
Chanjo zote mbili ni za MVA-BN zinatengenezwa na kampuni ya Bavarian Nordic ya Denmark.
Dozi hizi zimenunuliwa na kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Africa CDC na kutolewa na Marekani.
“Chanjo hizo zitahifadhiwa Kinkole Hub, kituo cha kuhifadhi chanjo katika mji mkuu wa Kinsasha, kabla ya kupelekwa maeneo husika.” Dk. Cris Kacita, meneja wa kudhibiti mpox wa DRC alisema.
Chanzo: BBC Swahil