TAASISI INAYOFUNZA PANYA KUPIMA VIMELEA VYA TB YAJIPANGA KUISHAWISHI WHO KUIDHINISHA NJIA HIYO KUWA RASMI TANZANIA

Moja ya panya wanatumika kupima TB
Happiness Tesha, Kigoma
Taasisi ya APOPO inayoendesha mradi wa Panya wanaotumika kugundua virusi vya ugonjwa Kifua Kikuu(TB), nchini Tanzania imejipanga kufanya utafiti wa kupima usahihi wa matokeo ya vipimo vinavyofanywa na Panya wao kugundua vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu ili kulishawishi Shirika la Afya Duniani(WHO), kuthibitisha panya kama njia rasmi ya kupima ugonjwa huo.
Matarajio ya APOPO ni kuwa utafiti huo utafikia asilimia 90 ya usahihi wa matokeo ya vipimo vinavyofanywa na Panya.
Upimaji wa vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu TB kwa njia ya Panyaunafanywa na Panya ambao wamefundishwa kunusa sampuli za makohozi ya watu ili kubaini ugonjwa huo.

Moja ya panya wanatumika kupima TB
Kutokana na uwezo wao mkubwa wa kunusa, panya hao wameweza kutambua sampuli zenye vimelea vya TB hata pale ambapo njia za kawaida zilishindwa, kwa mujibu wa Dkt Joseph Soka ambaye ni Meneja wa program ya Panya wanaopima TB Tanzania chini ya shirika la APOPO.
“Sasa teknolojia yetu hii tulifanya utafiti wa kupima usahihi wake mwaka 2014 tukagundua ni kwa asilimia 78 kwa hiyo tunataka kufanya utafiti kwa kuangalia setting nyingine ili kuona kama usahihi wake unawezakufika asilimia 90, anasema Dkt Joseph Soka.
Dkt Soka anaeleza kuwa ili Shirika la Afya Duniani WHO liidhinishe njia fulani ya kupimaugonjwa ni lazima njia hiyo itoe usahihi wa asilimia 90 katika majibu, licha ya ukweli kwamba njia zinazotumika sasa kupima TB hazijafikisha asilimia 90.

Mwalimu na mlezi wa panya akiwa anafanya utambuzi wa sampuli za makohozi yenye vimelea vya TB katika chumba cha maabara.
Anasema wanajua kwamba teknlojia ya Hadubini usahihi wake haujawahi kufika hata asilimia 50 lakini WHO iliidhinisha kutumika kwa ajili ya matumizi ya kupima makohozi, hata gene expert ambayo ni teknolojia inayotumia molecular kupima vinasaba haijawahi kufika asilimia 90.
Dkt Soka anasema Matumizi ya Panya katika kupima vimelea vya ugonjwa KifuaKikuu kwenye makohozi ya mtu yamethibitisha tija nyingi zaidi kwa mujibu wa Dkt Soka hasa eneo la gharama na muda wa vipimo.
Panya mmoja ana uwezo wa kupima sampuli 100 ndani ya dakika 10 hadi 20, sampuli hizo hizo zitachukua siku 4 za kazi kwa mtaalamu wa maabara kuweza kuzipima na kutoa majibu, lakini pia gharama.
Panya anatumia dola 1.13 wakati teknolojia kama ya Hadubini inatumia zaidi, wakati Gene expert ambayo ndio inatumika kwa sana inatumia dola 20, mashine moja ya gene expert inagharama siochini ya dola 30,000.
Hivi sasa pia taasisi ya APOPO inafanya tafiti nyingine za kuwatumiapanya Panya hawa kupima TB kwa aina nyingine ya sampuli tofauti na makohozi, ambapo sasa wanataka kutumia Jasho, Mkojo, Mate ama kinyesi kugundua vimelea vyaKifuakikuu.