ZITTO KUWASILI KIGOMA KESHO KWA KAZI MAALUMU

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT wazalendo Mh. Zitto Kabwe anatarajia kuwasili mkoani Kigoma mapema kesho kwa ajili ya kushiriki na kuunga mkono shughuli mbalimbali za kichama ambazo zitatekelezwa mkoani humo.

Mh. Kabwe atawasili katika uwanja wa ndege wa mkoa wa Kigoma majira ya saa mbili asubuhi na kushiriki dua maalum ya kuombea uchaguzi wa serikali za mitaa kuanzia saa nne kamili asubuhi.

Hata hivyo Mh. Kabwe atazindua ngome ya chama hicho katika eneo la mwanga sokoni na majira ya jioni atakuwa na mkutano wa hadhara katika soko la Noti lililopo eneo la Ujiji.

 

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )