CCM YAMPITISHA RAIS SAMIA KWA 100% KUGOMBEA URAIS 2025.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa wamempitisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Tanzania, kuwania nafasi hiyo kwa muhula mwingine katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumapili Januari 19, 2025 msimamizi wa uchaguzi huo, Dk Tulia Ackson amesema wajumbe 1,924 wote wamepiga kura ya ndiyo kwa Rais Samia huku makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dr Hussein Mwinyi akimtangaza Rais Samia kuwa mgombea rasmi wa Urais.
Aidha mkutano huo umempitisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kuwa mgombea urais kwa chama hicho kwa upande wa Zanzibar katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa upande mwingine Halmashauri Kuu CCM imempitisha Balozi Emannuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Akitangaza jina hilo, Rais Samia amesema alipokea barua kutoka kwa Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ambaye ameomba kupumzika katika nafasi hiyo baada ya kipindi chake cha miaka minne ofisini