LISSU MWENYEKITI MPYA CHADEMA, AMNG,OA MBOWE

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam

Matokeo ya jumla ya uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yametangazwa huku Tundu Lissu akiibuka kidedea.

Katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, wapigakura waliojisajili walikuwa 1,014 kura zilizopigiwa ni 999, halali zikiwa 996 na tatu zimeharibika.

“Odero Odero kapata kura moja sawa na asilimia 0.1, Freeman Mbowe amepata kura 482 sawa na asilimia 48.3 huku Lissu akipata kura 513 sawa na asilimia 51.5,” amesema Profesa Raymond Mushi mwenyekiti wa uchaguzi.

Nafasi ya Makamu mwenyekiti wa Chadema Zanzibar ameshinda Said Mzee Said ambaye amepata kura 625 sawa na asilimia 89 ya kura 706 huku halali zikiwa 700 na sita zimeharibika.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )