TUME YA HAKI ZA BINADAMU KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA KIGOMA UJIJI
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora inatarajia kufanya Mikutano ya hadhara kwa Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ameyasema hayo Kamishina wa Tume ya Haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora Mhe. Amina Talib Ali Februari 10, 2025 alipofanya mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Amesema Wataalamu wapo Mkoani Kigoma kutoa elimu kwa Watendaji wa Serikali na kukutana na Wananchi kwa kufanya mikutano ya hadhara ili kutoa ushauri na kupokea malalamiko ya uvunjifu wa haki za binadamu na kuelewa Misingi ya Utawala Bora.
Pia mikutano hiyo itafanyika kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
Amesema mara baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi tume inatoa siku tisini (90) kwa Uongozi wa Mkoa na Wilaya kupata mrejesho na kutoa majibu ya malalamiko ya Wananchi.