WAJAWAZITO KATA YA BUHANDA KIGOMA UJIJI WASOGEZEWA HUDUMA YA UPASUAJI

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Wananchi wa kata ya Buhanda Manispaa ya Kigoma Ujiji wameondokana na adha ya kufuata huduma za upasuaji katika hospital ya rufaa ya maweni na vituo vingine vya afya baada ya kituo cha afya cha kata hiyo kuanza kutoa huduma ya upasuaji kwa Wajawazito wanaopata uchungu pingazi.

Huduma hiyo imeanza kutolewa Februari 14, 2024 mara baada ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kuwezesha vifaa tiba vya zaidi ya shilingi Million mia tatu (Tsh Million 300/=) katika kituo hicho cha afya.

Huduma hiyo ya upasuaji ya kwanza imesimamiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa Dr. Hashim Mvogogo chini ya Dr. Festus Bavuma, Dr Ally Said Abdallah, na Mtaalamu wa dawa za usingizi Pastory Simon huku mtoto wa kiume akizaliwa.

 

 

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )