WAZIRI MKUCHIKA AANZA ZIARA MKOANI KIGOMA KUKAGUA UTEKEKEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

WAZIRI wa nchii Ofisi ya Raisi Ikulu (Kazi Maalum) George Mkuchika amesema kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza na kukamilisha miradi yote ya miundo mbinu mkoani Kigoma ili kurahisisha upatikanaji huduma mkoani humo na nchini kwa ujumla.

Waziri Mkuchika alisema hayo akiwa  Manispaa ya Kigoma Ujiji alipoanza  ziara ya siku nne mkoani hapa kutembelea miradi na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi kueleza kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Raisi Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuchika ametembelea mradi wa maboresho na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma, kutembelea bandari ya Kigoma na kukagua utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa meli za Mv.Liemba na MT Sangara na kusema kuwa miradi yote ambayo serikali inatekeleza itakamilishwa.

Waziri huyo alisema kuwa kwa sasa ndege za Shirika la Ndege (ATCL) zinafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kupitia Kigoma hadi Bujumbura mara tatu kwa wiki na hiyo yote inawezesha wananchi wa nchi hizo mbili kusafiri bila kuzuizi wala shida zozote na kufanya kuwa na mwingiliano mkubwa wa shughuli za biashara na kijamii baina ya nchi hizo.

Aidha alibainisha kuwa ukarabati wa meli ya abiria ya Mv.Liemba unaendelea na serikali itahakikisha ukarabati unakamilika na meli inafanya kazi mapema Zaidi ambapo ikikamilika itafanya safari katika  nchi zote za ukanda wa maziwa makuu zinazozunguka ziwa Tanganyika.

Awali Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuchika Meneja wa Wakala wa barabara  (TANROADS) mkoa Kigoma,Narcis Choma alisema kuwa Mradi wa uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Kigoma utahusisha jengo la abiria, ujenzi wa uzio wa uwanja, mnara wa kuongozea ndege na taa katika barabara za kuongozea ndege.

Choma alisema kuwa mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 46.6 na kutekelezwa chini ya kampuni ya China Railways Engineering.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )