UVINZA WAZINDUA UGAWAJI WA MITUNGI YA GESI.

Na Mwandishi Wetu, Uvinza – Kigoma

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh. Dinah Mathamani amezindua Ugawaji wa mitungi ya gesi kwa gharama ya elfu ishirini (20) kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.

Uzinduzi wa Ugawaji wa mitungi ya gesi kwa Wilaya ya Uvinza umefanyika katika kata ya Nguruka na Itebula katika viwanja vya eneo la posta Nguruka tarehe 15 April,2025.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mh.Dinah amesema Ugawaji wa mitungi ya gesi ni utekelezaji wa kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi, uboreshaji wa Afya za wananchi na utunzaji wa Mazingira kwa kupunguza matumizi ya Kuni.

” Mitungi hii ya gesi inatumiwa na akina mama japo na wakina baba wanatumia, hivyo ni jukumu la Kila mwananchi kuhakikisha anatunza Mazingira kwa kutumia Nishati Safi ya kupikia” alisema Mh. Dinah.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi wameishukuru Serikali kwa kuwagawia mitungi ya gesi kwani zitawasaidi kurahisisha kupika kwa haraka hata wanapotoka mashambani na Sasa watapunguza matumizi ya mkaa na kuni.

Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )